NYOTA YA WACHEZAJI WA TANZANIA YAWAKA UBELGIJI
Himid Mao ’Ninja’ ametua nchini Ubelgiji na kupokelewa na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.
Samatta anakipiga katika kikosi cha KRC Genk cha Ubelgiji wakati Mao alikuwa nchini Denmark ambako amekwenda kufanya majaribio katika kikosi cha Randers.
Wakati tayari Himid ameshacheza mechi moja ya kirafiki kwa ajili ya majaribio, leo ameonekana katika picha baada ya kuwasili nchini Ubelgiji.
Samatta ameeleza kumpokea Himid ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi cha Taifa Stars na Samatta ndiye nahodha.
Post a Comment