MYATE AFUNGUKA MAZITO KUHUSIANA NA TETESI ZA KUHAMA SIMBA..
WAKATI Pastory Athanas amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili, winga mwingine wa Simb,a Jamal Mnyate amesema bado yupoyupo Simba.
Jana timu hiyo ya Singida imemtambulisha Athanas ambaye Simba walimsajili kutoka Stand United ya Shinyanga katika usajili uliopita wa dirisha na akawa hana nafasi ya kutosha katika wekundu hao wa Msimbazi.
Lakini kwa upande wake Mnyate ambaye naye majeruhi yalimfanya akose kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba, amefunguka na kusema bado ataendelea kuweko kwenye klabu hiyo kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mnyate alisajiliwa na Simba kutoka timu ya Mwadui kwa mkataba wa miaka miwili lakini tangu aliposajiliwa alifanikiwa kucheza mechi kadhaa kutokana na mara nyingi kuwa anasumbuliwa na majeruhi.
“Kwa hivi sasa ni ngumu kusema msimu ujao nitakuwa wapi kwasababu bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Simba, kikubwa mimi nawasikiliza wao waajili wangu watakavyonambia kuhusu hatima yangu,” alisema.
Mnyate alisema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kutokana na kuwa bado yupo chini ya mkataba angekuwa huru kusema msimu ujao angeenda timu gani.
Aidha Mnyate amewapongeza viongozi wake kwa usajili walioufanya kwa kuwarudisha wachezaji wao wa zamani kama Emmanuel Okwi, Shomary Kapombe ambao walikuwa tishio Ligi Kuu.
Post a Comment