MOTO WATEKETEZA SOKO LA MWEMBE TAYARI DODOMA
Moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia Aprili 29,2017 umeliteketeza soko la Mwembe Tayari Katika Manispaa ya Dodoma na kusababisha hasara kubwa ikiwemo ya spea za magari kugeuka kuwa vyuma chakavu na mali mali nyingine kuwa majivu.
Mmiliki wa kibanda cha spea Yohana Juma aliyekuwa tayari na mzani wa kupimia vyuma chakavu amesema wamepata hasara kubwa kwakuwa biashara ya spea inatumia mtaji mkubwa.
Naye Makamu Mkwenyekiti sokoni hapo bwana Aloyce amesema vibanda vilivyoteketea pamoja na mali ni 70 huku akitaja aina ya biashara zilizokuwa zikifanyika sokoni hapo ambapo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni mama lishe.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mdeme aliyefika kujionea hali halisi amewapa pole na kuahidi kupeleka wataramu wa tathimin huku akiwaomba wasinyoosheane vidole.
Post a Comment