‘Tulijua matokeo kabla hata mechi haijaanza’ – Kocha Azam FC
Kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema, walikua wanajua kila kitu kuhusu mechi yao ya nusu fainali ya kombe la FA au Azam Sports Federation Cup dhidi ya Simba kabla hata ya mchezo kuanza.
Cheche amesema walishaanza kuona dalili mbaya kwao kuanzia kwenye mkutano kabla ya mechi (Pre-match meeting) na kilichokuja kutokea badae uwanjani hakikuwashangaza sana.
Azam wanambebesha mzigo wa lawama mwamuzi Mathew Akrama kwa kushindwa kuumudu mchezo huku kitendo cha mwamuzi huyo kumwonesha kadi nyekundu Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 16 tangu kuanza kwa mchezo kikipingwa vikali.
“Mchezo haukua mzuri kwa sababu ya mvua na maamuzi hayakua ya fair. Tangu tunatoka kambini kwetu tuliwaambia wachezaji wetu kuhusu haya yaliyotokea kwa sababu tulikua tunajua kilakitu kabla hata ya mchezo wenyewe.”
“Tangu tukiwa kwenye Pre-match meeting tulijua mchezo utakuaje. Wenyeji wa mpira wa Tanzania wanajua, wale waliokuja kwenye mpira wetu tangu miaka ya 1970 kuja hadi leo wanajua mpira wa Tanzania upoje.”
“Kadi nyekundu ya moja kwa moja iliyotoka mapema ndio iliyotuumuza na kutuchanganya, game plan yetu ikavurugika kabisa. Ukiachana na kadi nyekundu bado kulikua na vitu vidogovidogo ambavyo hatuwezi kuvizungumza, lakini tumeshashindwa basi tutajipanga kwa ajili ya mwaka ujao.”
Baada ya mchezo kumalizika, mwamuzi Mathew Akrama na wasaidizi wake ilibidi wapate ulinzi wa kutosha kutokana na kuzongwa na wachezaji wa Azam pamoja na viongozi wa benchi la ufundi waliokua wakilalamikia maamuzi yake.
Post a Comment