‘Goli la Amis Tambwe lilinitia aibu’ – Casillas


MLINDA mlango wa Kagera Sugar, Hussein Sharif ‘Casillas’ ameibuka na kusema kuwa alikuwa akimuogopa straika wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi kila alipokutana naye uwanjani.

Casillas ambaye msimu huu alipata majanga ya kusimamishwa na klabu yake ya Kagera Sugar kwa madai ya rushwa, amesema alikuwa akimuogopa Tambwe ili asimfunge.

Shaffihdauda.co.tzilizungumza na Hussein Sharrif ‘Cassillas’ amesema: “Ni straika ambae ni mjanja na pia msumbufu akiwa na mpira ni lazima akufunge tu.”

“Msimu uliopita nilipokuwa Mtibwa Sugar sikutaka hata siku moja Tambwe
anifunge,lakini walivyokuja kucheza na sisi Morogoro akanifunga nilijisikia aibu kwa sababu kabla ya mpira kuanza nilimwambia leo hunifungi,”amesema Casillas.

Mchezaji huyo ambae kwa sasa anakipiga katika timu ya Burudani FC inayoshiliki michuano ya Sport Extra Ndondo Cup ambayo yapo chini ya Cloud Media Group.

No comments

Powered by Blogger.