Kilichomuondoa Ronaldo kutoka Real Madrid ni hiki hapa.



Sahau kuhusu Cr7 huyu ni Ronaldo mwenyewe mwenyewe De Lima ambaye naye aliwahi kukipiga katika klabu ya Real Madrid kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo.

Mabao 104 aliyoifungia Real Madrid yalitosha kabisa kumfanya balozi wa timu hiyo ya Hispania, muda mfupi baada ya yeye kustaafu katika soka.

Lakini nyuma ya pazia imegundulika kwanini Ronaldo De Lima aliamua kuondoka Real Madrid na inaonekana wazi hakuondoka kwa kupenda katika klabu hiyo.

Ronaldo anasema aliongezeka kilo na kocha wake wa kipindi hicho Fabio Capello hakupendezwa kabisa na suala hilo ndipo wakaanza kupishana.

Ronaldo amekiri kwamba ni kweli kilo ziliongezeka lakini hiyo haikumfanya yeye kuacha kufunga uwanjani lakini bado Capello hakupenda suala hilo.

“Sikutaka kuondoka, muda mwingine kama kocha anakuwa na majukumu yake na kuongezeka uzito ni jambo la kawaida ilimradi tu uwe unafunga mabao” alisema Ronaldo.

Ronaldo ambaye hakuwahi kushinda kombe la champions league amewahi kushinda kombe la dunia lakini pia amewahi kukipiga na klabu ya Barcelona na Ac Millan.

No comments

Powered by Blogger.