Kumbe-Dida-wa-Times-mdomo-wa-bure afunguka haya
MTANGAZI wa kipindi cha “Mitikisiko ya Pwani” cha Times Fm, Khadija Shaibu “Dida” ameweka wazi kuwa “mdomo” wake huishia studio anakosikika akitangaza kwa mbwembwe na mikwara, ambapo amesema kuwa hana ubavu wa kupigana kama wengi wanavyodhani. Akiongea na saluti5, Dida amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakimchukulia kama mwanamke mshari anayependa ugomvi, huku akiwa na nguvu za kuzichapa na yeyote atakayelianzisha kwa wakati anaotaka. “Mimi bwana sina nguvu za kupigana, tena naogopa kabisa ngumi. We ukitaka kujua kuwa mi ni mwoga jaribu kuchokoza ugomvi mbele yangu uone nitakavyotimua mbio na kukuachia vumbi nyuma,” amesema Dida. “Tena usije ukajishaua kuchokozana na mtu huko halafu eti ukategemea una dada yako Times Fm sijui anaitwa Dida, lako hilo. Ukinipigia simu nitaitika kama niko usingizini vile na nitazuga nimelala kabisa,” aliongeza mtangazaji huyo mwenye maneno mengi.
Post a Comment