Majeruhi wa Shule ya Lucky Vicent kupelekwa Marekani kwa matibabu


 Jopo la madaktari bingwa wa Shirika la Stemm la Marekani kwa kushirikiana na Serikali, limeamua kuwapeleka  Marekani kwa matibabu majeruhi watatu  wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.

Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru ni Jofrey Tarimo, Doreen Mshana na Sadia Awadh wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Marekani wakiambatana na wazazi wao,  daktari na muuguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha.

Matibabu hayo  yatatolewa kwa  ufadhili wa madaktari hao kutoka Marekani ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasidia wanafunzi hao kutoka kwenye gari lililo pata ajali, wakiwa njiani kuelekea Ngorongoro na Serengeti kutalii.
Daktari mkuu wa hospitali Mount Meru,  Wonanji  Thimos  amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na madaktari hao imeshaanza taratibu za kuwasafirisha majeruhi hao kwa ajili ya matibabu zaidi.


Dk Thimos amesema taratibu za safari zikikamilika majeruhi hao watasafirishwa kwenda Marekani wakati wowote kuanzia sasa
post-feature-image

No comments

Powered by Blogger.