MALAIKA MPYA’ MAN UNITED: ANGEL GOMES, MIAKA 16, AZUA GUMZO ULAYA!


JOSE MOURINHO alishatoboa kuwa kwenye Mechi yao ya mwisho kabisa ya EPL, LIGI KUU ENGLAND, hapo jumapili dhidi ya Crystal Palace ambayo haina maana yeyote kwao atachezesha Kikosi mchanganyiko chenye Chipukizi kadhaa na mmoja kati ya hao ni Angel Gomes ambae Juzi alizoa Tuzo ya Klabu ya Manchester United ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana.

Uamuzi huo wa Mourinho wa uteuzi wa Kikosi cha Mechi hiyo ya EPL ambayo matokeo yake yeyote hayatabadili Nafasi yao ya 6 hasa unalenga kulinda Mastaa wao kwa ajili Fainali ya Jumatano ya huko Stockholm, Sweden ya UEFA EUROPA LIGI ambayo watapambana na Ajax Amsterdam ya Netherlands.

Miongoni mwa Chipukizi ambao wametajwa Kikosini:

MAKIPA: Kieran O'Hara (Miaka 21), Joel Castro Pereira (20).

BEKI: Demetri Mitchell (20).

VIUNGO: Zachary Dearnley (19), Angel Gomes (16), Josh Harrop (21), Scott McTominay (20), Matthew Willock (20).

Kati ya wote hao, huko Uingereza, Angel Gomes, Kijana wa Miaka 16, Mpwa wa Winga wa zamani wa Man United Nani, ndie amezua gumzo kubwa hasa baada ya Juzi kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana.

++++++++++++++++

WASIFU:

Jina: Angel Gomes

Umri: 16

Kuzaliwa: London

Pozisheni: Attacking midfielder

Klabu: Manchester United

Kimataifa: England U-16 na U-17

++++++++++++++++

Kwa kuzoa Tuzo ya Man United ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana, ambayo inaitwa Jimmy Murphy Youth Team Player of the Year, Angel Gomes ameweka Historia ya kuwa Kijana mwenye Umri mdogo kabisa kuibeba.

Miongoni mwa Wachezaji maarufu waliowahi kuchukua Tuzo hii ni pamoja na Paul Scholes na Ryan Giggs.

++++++++++++++++

Washindi wenye Umri Mdogo kutwaa Tuzo ya Man United ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana:

Angel Gomes – Miaka 16 Miezi 9 - 2017

Mats Daehli – Miaka 17 Miezi 2 -2012

Will Keane – Miaka 17 Miezi 4 - 2010

Phil Neville – Miaka 17 Miezi 4 - 1994

Axel Tuanzebe - Miaka 17 Miezi 6 - 2015

Ryan Giggs – Miaka 17 Miezi 6 - 1991

Danny Welbeck – Miaka 17 Miezi 6 - 2008

Federico Macheda - Miaka 17 Miezi 9 - 2009

Gomes hucheza kama Kiungo Mshambuliaji na Msimu huu amepiga Bao 12 katika Mechi 19 alizoanza.

Gomes pia huzichezea Timu za Taifa za Vijana za U-16 na U-17.

Kijana huyu alizaliwa Jijini London na Baba yake pia aliwahi kuwa Mchezaji ambae alitwaa Ubingwa wa Ulaya wa U-17 akiichezea FC Porto ya Ureno Mwaka 1989 na kisha kuhamia Klabu kadhaa Duniani ikiwemo Salford City ya huko Jijini Manchester.

Gomes alisainiwa na Man United akiwa na Miaka 13 na uwezo na kipaji chake kilimfanya amudu kuchezea Kikosi cha U-18 akiwa na Miaka 14 tu.

Mwaka 2015, Gomes alishinda Tuzo ya Mchezaji wa Thamani kwenye Premier Cup ambako huko England hushindaniwa na Vikosi vya Chipukizi vya Klabu kubwa.

Nicky Butt, Kiungo wa zamani wa Man United ambae sasa ndie anasimamia Kikosi cha Vijana cha Man United, ameeleza: “Angel Gomes ni Kijana mwenye Kipaji kikubwa mno na tuna matumaini makubwa mno kwake!”




No comments

Powered by Blogger.