MAMIA YA WATU JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WAPOTEZA MAISHA.

Makundi yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya kati yamewaua raia wasiopungua 45 katika mapigano ya kisasi katika muda wa miezi mitatu iliyopita wasimamizi wa haki za binadamu walisema katika ripoti ya siku ya Jumanne.
Menschen fliehen aus Zentral-Afrika (Reuters)
Watoto wakimbia vurugu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati
Vurugu hizo zilisabishwa na mashambulizi ya vikundi vyenye silaha, zilisambaa  kati ya mkoa wa Ouaka, ambayo ni mpaka baina ya waislamu wa kaskazini na wakristo wa kusini nchini humo.
"Mvutano wa madaraka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati umewafanya wananchi wa kawaida kutoka pande zote kuathirika na mashambulio yanaoyofanyika," alisema Lewis Mudge, mtafiti wa mambo ya Afrika katika taasisi ya usimamizi wa haki za binadamu huko Marekani.
Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa ikikabiliwa na vurugu la kisiasa tangu 2013 wakati kundi la waasi wa Seleka lililokuwa na wapiganaji wengi Waislamu lilipomng'oa madarakani rais Francois Bozize. Kundi hilo liliendelea kuuwa na kufanya  mashambulio, jambo ambalo liliwafanya wakristo nchini humo kuanzisha makundi na kijeshi ya kujilinda.
Hata baada ya uchaguzi wa kidemokrasia na kuapishewa kwa rais Faustin-Archange Touadera
March 2016 kundi la Seleka na makundi mengine yanaendelea kufanya vurugu nchini humo.
Mtu mmoja aliyeshuhudia shambulio la hivi karibuni, anayejulikana kwa Clemnet tu, alisema
wapiganaji wa kundi la Fulani Union for Peace Afrika ya katiyaani Umoja wa Fulani kwa ajili ya amani, waliwapiga risasi watoto wanne na kuwauwa akiwemo mtoto wa miezi saba katika shambulio la mwezi wa Machi.
Wasimamizi wa haki za binadamu waliwafanya mahujiano na wakaazi kadhaa wa mji wa Barbaric mwezi wa April. Wazimamizi hao walisema kuwa kiwango cha watu walioathirika imepanda kidogo kwa sababu bado kuna wale watu waliopotea.
Umoja wa Mataifa ambao una walinda usalama 13000 katika nchi hiyo, ambayo ni koloni la zamani la Ufaransa. Wajumbe hao wamejaribu kufanya mashambulizi ya anga ili kuondoa makundi yanayofanya mashabulizi  huko Ouaka na kuendelea kuingia Barbaric.
Zentralafrikanische Republik Bangui Minusca UN-Truppen (picture-alliance/AA/)
Walinda usalama wa Umoja wa Mataifa
Lakini bado vurugu zinaendelea nchi humo. Kundi la kutoka tiba za msaada la MS lilisema kuwa mwezi uliopita ulikuwa ni mwezi mbaya wa mashambulizi uliokuwa haujapata kutokea kwa muda mrefu. Kundi hilo pia liliripoti kuwepo kwa mauaji ya kikatili ya kukatakata na ya kunyonga.

No comments

Powered by Blogger.