MANJI AMWAGA MANYANGA BARUA YAKE YALETA SIMANZI KUBWA KWA WANA YANGA



Barua iliyosainiwa na Yusuf Manji Mei 22, 2017 inaonesha kwamba Manji ameachia rasmi nasasi ya uenyekiti wa klabu ya Yanga na makamu mwenyetiki wa klabu hiyo Clement Sanga atakuwa mwenyekiti na kuiongoza klabu hadi hapo uchaguzi utakapofanyika ili kumpata mwenyekiti mpya.

Kwa mujibu wa maelezo ya barua, Manji alifikia uamuzi wa kujiuzulu Mei 20 mwaka huu siku ambayo Yanga ilitangazwa kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2016/2017.

Katika barua hiyo, Manji amsema ameamua kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa wengine nao kushika uongozi ndani ya klabu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.