Maskini Marco Reus, fainali yamponza
Luke Shaw ni kati ya wachezaji vijana wadogo ambao suala la majeruhi limekuwa likitia shaka kuhusu maisha yao katika mpira wa miguu kwank kila akirudi uwanjani anaumia.
Sasa Ujerumani nako kuna Marco Reus, Reus naye kama ilivyo kwa Luke Shaw amekuwa akitumia muda mwingi nje ya uwanja kuliko ndani ya uwanja kutokana na majeraha.
Lakini mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwepo uwanjani akiisaidia Borussia Dortmund kubeba ubingwa wao wa kwanza toka kocha Jurgen Klopp aondoke katika klabu hiyo.
Reus alianza katika mchezo huo ambao Dortmund waliibuka kidedea cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Eintracht Frankfurt lakini alishindwa kuendelea na mchezo huo baada ya kupata majeraha.
Japokuwa baadae Reus alionekana akishangilia kombe na wachezaji wenzake lakini ripoti za madaktari zinaonesha Reus huenda akakaa tena nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Ripoti za madaktari zinasema kutokana na majeraha aliyoyapata Reus anaweza kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha kuanzia wiki tisa hadi 10.
Kama unakumbuka hii sio mara ya kwanza kwa Reus kupata majeraha makubwa kwani mwaka 2014 wakati wa kombe la dunia aliumia na mwaka 2016 alikosa michuano ya Euro kutokana na majeruhi.
Post a Comment