NITABAKI MADARAKANI MPAKA MUDA WANGU UISHE.."JACKOBO ZUMA"
Rais wa Afrika Kusini anayekumbwa na kashfa Jacob Zuma, ameondoka kwenye mkutano wa siku ya kimataifa ya wafanyazi baada ya kukemewa na wafanyakazi wanaomtaka ajiuzulu.
Fujo zilizuka kati ya wafuasi wa Bwana Zuma na wapinzani na kusabababisha hotuba yake kufutwa.
Chama kikuu cha wafanya kazi Cosatu, kilimtaka Bwana Zuma ajiuzulu mwezi uliopita baada ya kumfuta kazi waziri wa fedha alijekuwa akiheshimiwa sana.
- Waandamanaji wanakusanyika kumpinga Zuma
- Rais wa zamani Afrika Kusini ampinga Jacob Zuma
- Zuma atuma vikosi vya jeshi kulinda bunge
Bwana Zuma ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019.
Alionyeshwa na runinga akiondoka jukwaani kwa hasira na kuondolewa na magari kutoka kwa mkutano ulioandaliwa mjini Bloemfontein
Maafisa wa vyeo vya juu wa ANC nao walikemewa kwenye mkutano uliofanyika mjini Durban.
Shinikizo za kumtaka Zuma ajiuzulu zimekuwa zikoongezeka tangu amfute kazi waziri wa fedha Pravin Gordan mwezi Machi.
Post a Comment