Rais Magufuli Amteua Simon Sirro Kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzabia Dkt. John Magufuli, amemteua kamishina wa polisi Simon Sirro kuwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP).
Kabla ya uteuzi huo IGP Simon Siro alikuwa kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam.
IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu kiongozi balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa leo Jumatatu katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam.
Post a Comment