ZABALETA AAGWA CITY, CARRICK KUBAKI OLD TRAFFORD!

MANUNITED-CARRICK-ABEBA-FACUPWAKATI Manchester City Jana wakimuaga Beki wao mkongwe Pablo Zabaleta amvae anaondoka Klabuni mwishoni.mwa Msimu, habari kutoka huko Manchester United zimesema kuwa Kiungo wao Mkongwe Michael Carrick ataongezwa Mkataba wa Mwaka Mmoja ili abaki kwa Msimu ujao.
Jana huko Etihad, Pablo Zabaleta aliagwa kwa kishindo wakati City inaichapa West Brom 3-1 katika Mechi ya EPL, LIGI KUU ENGLAND

Zabaleta, Mchezaji mwenye Miaka 32 kutoka Argentina, ameitumikia City kwa Miaka 9 na Jana aliingizwa kucheza Dakika ya 62 na kukaribishwa kwa shangwe.
Zabaleta ndie alieteuliwa Mchezaji Bora wa Mechi hiyo aliyoimaliza kama Kepteni baada kukabidhiwa Utepe wa Nahodha kutoka kwa Kepteni Vincent Kompany ambae alipumzishwa.
Mara baada ya Mechi kwisha, Zabaleta, ambae ni Mchezaji wa 3 kwa Utumishi wa muda mrefu nyuma ya Joe Hart na Kompany, alitoa Hotuba akiwa Uwanjani pamoja na Mkewe na Mwanawe na kisha kusindikizwa na Gwaride la Heshima la Wachezaji wenzake.
HUKO Old Trafford, zipo habari kuwa Kiungo Michael Carrick yuko mbioni kuongezewa Mkataba ili abaki kwa Mwaka Mmoja zaidi.
Carrick, mwenye Miaka 35, anatimiza Misimu 11 hapo Man United na Juni ipo Mechi Maalum ya kuuenzi Utumishi wake uliotukuka.
Carrick alijiunga Man United kutoka Tottenham Mwaka 2006 kwa Dau la Pauni Milioni 18.6.
Tangu wakati huo, Carrick ameichezea Man United Mechi 457 akifunga Goli 24 na yeye ni Namba 17 kwenye Listi ya Wachezaji waliotumikia muda mrefu.
Kwenye utumishi wake na Man United, Cartick, ambae pia alikuwa Mchezaji wa Kimataifa wa England, alitwaa Ubingwa wa England mara 5, UEFA CHAMPIONZ LIGI, FA CUP na Kombe la Ligi mara 2.

No comments

Powered by Blogger.