Arsene wenger atupia jiwe la euro 100m kwa kiungo huyu..........


Arsene Wenger haondoki Arsenal na bado atakaa katika klabu hiyo kwa miaka miwili zaidi na hii inamaanisha atakaa katika klabu ya Arsenal hadi mwishoni mwa mwaka 2019.
Wenger amekuwa akinyooshewa vidole kutokana na aina ya wachezaji anaowasajili kuonekana kama sio aina ya wachezaji ambao wanaweza kupigania ubingwa.
Wenger tofauti na Jose Mourinho au Pep Gurdiola ambao hutumia pesa nyingi sana kutafuta wachezaji ambao wanawataka na wachezaji wakubwa.
Arsene Wenger anaaminj zaidi katika vijana na hata wachezaji anaopendelea kusajili ni vijana ambao hata bei yao sokoni huwa sio kubwa tofauti na wachezaji wakubwa.
Aina ya usajili ya Wenger imekuwa ikiisaidia Arsenal katika upande wa kifedha kwani babu huyo amekuwa mchumi lakini inawaumiza sana uwanjani haswa linapokuja suala la kushindana na vilabu vikubwa.
Lakini Wenger amechoka kwani habari zinadai Wenger anajiandaa kutuma ofa ya kiasi cha £100m kwa Monaco ili kumsajili Mfaransa Kylian Mbappe.
Ni wazi na ni rahisi kwa Wenger kuuziwa Mbappe kutokana na kwamba Mbappe ni Mfaransa na wachezaji wengi wa taifa hilo wamekuwa wepesi kujiunga na Arsene Wenger.
Bado usajili unaendelea labda tusubiri tuone Mfaransa huyo atafanya nini katika kipindi hiki cha usajili ukizingatia kwamba anatoka kupata presha kubwa kutokana na matokeo aliyoyapata msimu uliopita.

No comments

Powered by Blogger.