Kamusoko na Ngoma wawafuta machozi viongozi ya Yanga
KIUNGO Thaban Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma wametuliza mzuka baada ya kuwaambia mabosi wa Yanga kwamba wapo tayari kubaki kwa muda zaidi katika kikosi hicho
. Taarifa zilizoifikia kabasele news zimesemsema Kamusoko amesema anakuja nchini wiki hii kumalizana na Yanga baada ya mafanikio katika mazungumzo ya kuongeza mkataba zaidi.
Kiungo huyo fundi amesema anataka kubaki Yanga ambayo imempa heshima kubwa hasa baada ya hivi karibuni kurejeshwa katika kikosi cha taifa na kwamba haoni kama watashindwa katika mazungumzo ya mwisho yatakayofanyika hapa nchini mara baada ya kuwasili. “Nitakuja hapo Tanzania wiki hii, nimeshazungumza na viongozi na tuko katika sehemu nzuri.
Wana Yanga wasiwe na wasiwasi, hakuna kitakachoshindikana,” alisema Kamusoko. Wakati Kamusoko akiyasema hayo, mmoja wa mabosi wa usajili, amesema Ngoma amekubali kusaini mkataba mpya wa kubaki ambapo hatma yake nae itajulikana mara baada ya kuwasili.
Ngoma ambaye kwa sasa yuko kwao Zimbabwe kwa mapumziko, inaelezwa kiasi cha dola 40,000 kitatumika katika kumuongezea mkataba huo ambapo utakuwa mkataba wa pili kwake na Yanga.
Post a Comment