Kilichosababisha Juma Kaseja aondoke Simba 2008 na kujiunga na Yanga




Inawezekana ukataka kufahami ile ishu iliyotokea mwaka 2008 ya golikipa wa Kagera Sugar Juma Kaseja kuweka rekodi ya usajili kwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa ndani ya Tanzania kwa dau la Tsh milioni 36 kipindi yupo Simba na kwenda Yanga.

Katika mahojiano na Sports Bar ya Clouds TV Juma Kaseja amezungumzia namna ilivyokuwa mwaka 2008 akaamua kuondoka Simba na kujiunga na Yanga kwa uhamisho wa rekodi wa dola za kimarekani 30000 ambazo zilikuwa kama milioni 36 za kitanzania kwa mwaka 2008.

“Mara ya kwanza natoka Simba 2008 nakwenda Yanga mpaka naenda kusaini Yanga nilikuwa naongea na viongozi wa Simba, yaani nipo na viongozi wa Yanga nawaambia subirini kidogo natoka nje naongea na viongozi wa Simba jamani hee nimepewa dola 30000 mwaka 2008 zilikuwa kama milioni 36 nyie mnaweza mkanipa hiyo hela?”>>>Kaseja

“Wapo baadhi ya viongozi wa Simba wananiambia chukua hiyo hela sisi hatuna uwezo wa kukupa hadi leo wapo Friends Of Simba na Friends Of Simba si ndio wanaoiongoza Simba leo hii? wananiambia wewe chukua hiyo hela sisi hatuna uwezo wa kukupa”>>>Kaseja



“Kila siku ulikuwa unatupigia kelele tukutafutie timu uende nje sasa hiyo hela si sawa na nje chukua lakini mimi nawashukuru kwa sababu kama wangekuwa na roho mbaya au nini, leo hii ningekuwa na maisha ambayo sio mazuri kama nilivyo sasa hivi wakanitia ujasiri japo ilikuwa ni ngumu kwa sababu ya hofu nikasaini” >>>Kaseja

“Kingine kilichonifanya niende Yanga ni zile shutuma za unauza mechi, sasa kama Yanga nawauzia mechi wananinuaje? nikaenda nikacheza Yanga nimecheza Yanga na huku pia nasikia huyo Simba lakini Simba nao wananiambia wewe mkataba wako ukiisha itabidi urudi, basi nikarudi Simba nikachukua mzigo” >>> Kaseja

“Nimecheza tena Simba zikaanza tena huyu anakula hela Yanga, Simba nako nikaondoka nimekaa nusu msimu sichezi, Yanga wakaniambia bwana njoo chukua Milioni 40 hizi hapa nikasaini miaka miwili nikaenda kucheza sasa hizi tuhuma za kula hela nazo zilikuwa zinachangia kuhama” >>>Kaseja

No comments

Powered by Blogger.