Lindelof atua rasmi Machester united
Sentahafu wa timu ya taifa ya Sweden Victor Lindelof amewasili uwanja wa mazoezi wa Manchester United - Carrington, tayari kwa kukamilisha usajili wake kutoka Benfica ya Ureno.
Lindelof amewasili Carrington leo asubuhi huku usajili wake ukitegemewa kuigharimu Manchester United pauni milioni 30.7. United ilijaribu kumsajili Lindelof bila mafanikio katika dirisha dogo la Januari, lakini hatimaye sasa imemtia mkononi beki huyo anayetegemewa kuimarisha ukuta wa Jose Mourinho.
Post a Comment