PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG ATAENDELEA KUVAA JEZI ZA MISTARI YA NJANO ZA BORUSSIA DORTMUND.....
Pierre-Emerick Aubameyang hatauzwa na ataendelea kubakia Borussia Dortmund msimu huu, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Ujerumani.
Aubameyang amekuwa akihusihwa na klabu kadhaa kwenye usajili wa kiangazi hiki, huku Chelsea ikitawala vichwa vya habari kwa siku za karibuni hususan baada ya kumkosa Lukaku kutoka Everton.
Hata hivyo habari mpya ni kwamba mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon ataendelea kuvaa jezi za mistari ya njano na nyesi za Borussia Dortmund kwa msimu wa 2017/18.
Post a Comment