Serikali yatoa kibali cha kuajiri watumishi 15000 kuziba nafasi za watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki.


Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh.Angela Kairuki amesema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki katika zoezi lililofanyika nchi nzima la kuwabaini na muda si mrefu nafasi hizo zitajazwa.


Mh.Kairuki amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum Iringa mh.Rita Kabati aliyetaka kufahamu juu ya ujazwaji wa nafasi hizo ambapo amekiri upungufu huo umesababisha usumbufu mkubwa katika taasisi mbalimbali za umma hivyo kuwahakikishia wananchi kuwa tatizo hilo litakwisha hivi karibuni.


Katika hatua nyingine akijibu swali la Mbunge wa Mtwara mjini Mh.Maftaha Abdallah Nachuma aliyetaka uboreshwaji wa bandari ya Mtwara kwa kudai kuwa imesahaulika licha ya kuwa na kina kirefu katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati,Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mh.Edwin Ngonyani amesema serikali inampango wa kuboresha na kuendeleza bandari zote nchini ikiwemo bandari ya Mtwara ili kuipunguzia mzigo bandari ya Dar es Salaam.


Mh.Ngonyani amesema kuwa tayari serikali imeshatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa gati katika bandari ya Mtwara yenye urefu wa meta 350 itakayogharimu zaidi ya shilingi bilioni137 inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi 21.

No comments

Powered by Blogger.