Waziri wa mambo ya ndani azuia wanaohusika na ripoti ya pili kutosafiri nje ya nchi
Jana June 12, Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti ya pili ya mchanga wa madini ambayo imebaini uwepo wa mikataba mibovu inayoitia hasara serikali ambapo kamati imetoa mapendekezo 21 ikiwemo kuchukuliwa hatua kwa wote waliohusika na ubadhirifu huo.
Ripoti iliyonifikia muda huu kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewazuia wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutoka nje ya mipaka ya Tanzania hadi vyombo vya dola vitakapofanya kazi yake kwa mujibu wa agizo la Rais JPM.
Waziri Mwigulu amesema >>> “Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao. Hongera sana Mh. Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu
>>>Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu<<< Waziri Mwigulu Nchemba

Post a Comment