YANGA YAPAMBANA KWA HAJI MWINYI......
YANGA imeanza kufanya mambo kwa utulivu ambapo Jumamosi imefanikiwa kumbakisha beki wake wa kushoto Haji Mwinyi kisha ikamalizana na kiungo aliyetakiwa na kocha wao George Lwandamina na kuachana na Salmin Hoza.
Aliyefanya kazi hiyo ya kumsainisha Mwinyi, aliyekuwa akiviziwa na Azam na mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika, akisaidiana na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambapo beki huyo amesaini mkataba mpya wa miaka miwili
. Mwinyi aliyesafirishwa jana kutoka kwao Zanzibar na kufika jana mchana ambapo haraka jana hiyohiyo akakubali kubaki Yanga ambapo sasa anatafutiwa beki mwingine atakayechuana nae.
Wakati Yanga ikianza hivyo, tayari klabu hiyo imefanikiwa kumsajili kiungo wa Mbao, Pius Buswita na kufanikiwa kuwapigisha chenga Azam waliomnyakuwa Salmin Hoza ambaye alikuwa akitakiwa kusajiliwa Yanga kwa ziada tu
. Katika ripoti ya kocha, Lwandamina kiungo muhimu aliyekuwa akimtaka kutoka Mbao ni Buswita lakini Yanga ikawapigisha chenga Simba na Azam kwa kutangulia kufanya mazungumzo na Hoza ambaye walimkimbilia kisha kumwacha Buswita ambaye sasa ni mali ya Yanga
. “Tumemalizana na Mwinyi, tulimwita haraka na Jumamosi tukamalizana nae, amesaini mkataba mnono wa miaka miwili kwa hiyo hatuna mashaka nae tena,” alisema bosi huyo. Ukiacha Mwinyi pia tumemsajili kiungo fundi wa Mbao, Pius Buswita ambae ndie kiungo mwafaka tuliyekuwa tukimtaka lakini tulijua kwamba hizi timu nyingine zinasubiri kusikia nini Yanga wanataka kufanya ili wao wakimbilie sasa tulipomtaja Hoza wao wakakimbilia kumsajili lakini tukafanikiwa kumpata Buswite tuliekuwa na mipango nae.”
Post a Comment