CHELSEA WAJITOSA KWA MORATA...
Baada ya klabu ya Chelsea kumkosa Romelo Lukaku sasa klabu hiyo inakaribia kufanya kweli kwa mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata ambaye taarifa zinasema yuko katika makubaliano ya mwisho mwisho na Chelsea.
Katika kuonesha kwamba klabu ya Rb Leizpg imepania haswa kuwatosa Liverpool kuhusu kiungo wao Naby Keita wameikataa ofa ya £75m iliyotumwa na Liverpool kwa ajili ya kumnunua kiungo huyo.
Liverpool hao hao baada ya ofa yao ya £75m kukataliwa inasemekana wameanza kuangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller ili aweze kujiunga na majogoo hayo ya London.
Inasemekana klabu ya Paris Saint German imeshafanya makubaliano na mchezaji wa klabu ya Barcelona Neymar ambapo kwa sasa PSG itawapasa kulipa kiasi cha £222m katika dirisha lijalo la usajili ili kumnunua Neymar.
Matumaini ya klabu ya Manchester United kumpata Ivan Perisic yameanza kufifia baada ya klabu ya Inter Millan kutaja jina la winga huyo katika kikosi kinachosafiri kulekea nchini China kwenye pre-season.
Vilabu vya Crystal Palace na Sampdoria viko katika mpambano wa kumnunua kiungo wa Arsenal aliyekuwa Fc Bournamouth kwa mkopo Jack Wilshaire japo Arsenal wanaonekana kutaka kumbakisha klabuni hapo.
Post a Comment