Kamati ya utendaji ya TFF yakutana, yatoa maamuzi magumu kuhusu Malinzi
Kamati Kuu ya Utendaji ya TFF imekutana jana na kutoa maamuzi ya kuwasimika viongozi wa muda ambao wataziba nafasi zilizoachwa wazi na Rais wa Shirikisho hilo, Jamali Malinzi na Katibu mkuu wake Selestine Mwesigwa.
Aidha, majina yaliyopitishwa ni pamoja na Wallace Karia kuwa Kaimu Rais wa Shirikisho hilo huku Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi akiteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu.
Kamati hiyo imesema kuwa viongozi hao walioteuliwa watakaimu nafasi hizo mpaka pale mahakama itakapotoa maamuzi ya kesi inayowakabili Rais wa Shirikisho hilo, Jamali Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa.
Post a Comment