Msondo ngoma wapoteza mwimbaji mashuhuri.Shaaban Dede...
Mwimbaji mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Dede, mwanamuziki wa Msondo ambaye pia aling’ara na bendi za Mlimani Park “Sikinde”, Bima Lee na OSS, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari pamoja na figo.
Hamad Dede ambaye ni mtoto wa marehemu, ameiambia Kabaselenews kuwa baba yake amefariki asubuhi hii na kwamba watatoa taarifa baadae juu ya ratiba ya kila jambo.
“Baada ya kama masaa mawili tutakaa kama familia na kutoa taarifa rasmi ya msiba utakuwa wapi na mazishi ni lini ingawa kuna kuna zaidi ya asilimia 70 kuwa tutazika kesho,” alisema Hamad
. Onyesho la mwisho Dede kushiriki ni lile lililofanyika Travertine Hotel, Magomeni la mpambano wa Msondo na Sikinde Mei 20 mwaka huu.
Post a Comment