"NAJITUMA MWENYEWE LAKINI MOURINHO NDIYE ANAENIFANYA NIWE BORA ZAIDI" LUKAKU...


STRAIKA wa Manchester United, Romelu Lukaku amezidi kummwagia sifa kocha wake, Jose Mourinho baada ya kusema kuwa tayari ameshamfanya kuwa mchezaji aliyeiva.

Sifa hizo za Lukaku, 24, kwa Mourinho zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Everton kwenda kujiunga na Man United kwa ada ambayo inasadikika kuwa ni pauni mil 75.

Mwanzoni mwa wiki hii staa huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji aliweza kufunga bao lake la kwanza katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Salt Lake katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu ujao.

Baada ya kufunga bao hilo, Lukaku ambaye msimu uliopita aliweza kufunga mabao 25 katika michuano ya Ligi Kuu England, alisema kuwa Mourinho ambaye ni kocha wake wa zamani wakati akikipiga Chelsea, tayari ameshafanya aimarike zaidi


“nafahamu kile ambacho anaweza kukifanya ndani ya timu na ni mtu ambaye amekuwa akinisukuma,” staa huyo aliyaambia magazeti ya Uingereza. “vilevile nimekuwa nikijituma mwenyewe lakini yeye ndie anayenifanya kuwa mchezaji bora.

Nadhani nimejifunza mengi kutoka kwake na ninajivunia kwamba naweza kufanya kazi nae,” aliongeza straika huyo. “Nafurahi kwa bao langu. Lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya, sisi kama timu tunafahamu tunahitaji kuwa bora zaidi,” aliongeza.

No comments

Powered by Blogger.