"NCHI INAKAZANA KUJENGA MFUMO WA DEMOKRASIA KANDAMIZI KWA LENGO LA KUDHOOFISHA UPINZANI FREDRICK SUMAYE..
Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chadema, Frederick Sumaye amesema kuwa licha ya kukatazwa wasizungumze masuala '
'
ya kisiasa, lakini hawatanyamaza.
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Sumaye amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa niaba ya wananchi ambao wana imani nao.
Amesema nchi kwa sasa inakazana kujenga mfumo wa demokrasia kandamizi ambayo kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma maendeleo.
"Viongozi wa upinzani wamekuwa wakikamatwa, wanawekwa rumande, wanatishwa lengo ni kudhoofisha upinzani," amesema Sumaye.
Amesema licha ya juhudi hizo za kuwarubuni baadhi ya viongozi wakiwamo madiwani wachache, hawatadhoofika na wataendelea kufanya Kazi.

Sumaye amesema kwamba wanataka kujenga upinzani wa kweli wenye lengo la kusaidia wananchi.
Amesema katika kulihakikisha hilo hadi kufikia mwaka 2018 hakutakuwa na kijiji, mtaa utakaokuwa hauna tawi la Chadema
Post a Comment