TAMBWE AMUONEA HURUMA HANS POPPE SOMA HAPA ALICHOKISEMA.....

Mshambulizi mkongwe wa Yanga, Amissi Tambwe anamuonea sana huruma Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe.

Tambwe anamuonea Hans Poppe huruma kwa kuwa anaona kikosi cha Yanga, kiko vizuri na itampa Hans Poppe shida sana msimu ujao.

Kwani baada ya Ajibu kutua Yanga, Tambwe anaona Yanga itakuwa haishikiki msimu ujao!

Ajibu amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na kukabidhiwa jezi namba 10 atakayoitumia katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.


Unamuona Ajibu tunaye, katika ushambuliaji itakuwa shida sana. hapa namuone huruma Hans Poppe maana atakosa la kusema, tutafunga sana mabao,” alisema Tambwe.

Wengine wapya ambao wamesajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao ni kipa Youthe Rostand kutoka African Lyon, Pius Buswita (Mbao FC), Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (Taifa Jang’ombe), Gadiel Michael (Azam FC) na Raphael Daud kutoka Mbeya Cit
y.

No comments

Powered by Blogger.