Trump: Tumechoka kuivumilia Korea Kaskazini
Rais wa Marekani Donald Trump anasema muda wa uvumilivu wa kimikakati kwa Korea Kaskazini umekamilika sasa.
Katika hotuba ya pamoja na rais wa Korea Kusini Moon Jae, kwenye ikulu ya White house, Trump amesema kwamba vitisho vya Korea Kaskazini vinafaa kupata majibu ya kijasiri.
Hata hivyo, Trump amesema ni muhimu kuwe na ushirikiano katika kugawana mzigo wa kuhakikisha usalama.
Rais wa Korea Kusini amesema kwamba taifa lake litaweka marekebisho ya kiuslama na kujenga msingi dhabiti wa kujikinga.
Rais Moon pia amesema ni muhimu kuendelea na majadiliano na viongozi wa Korea Kaskazini.
Post a Comment