''NIKO TAYARI KURUDI MWADUI FC ENDAPO KOCHA ALIYEPO WAKIMFUKUZA''ALLY BUSHIRI......


Na Selemani Ussi, Unguja
Kocha Ali Bushiri amesema yuko tayari kurejea kuinoa Mwadui FC ambayo aliamua kuachana nayo.
 
Bushiri amesema amepokea simu kutoka Mwadui FC ambao wanamuomba arejee kuifundisha.  
Lakini ametoa kwamba kama ni kurejea, lakini anachotaka ni kuona uongozi wa Mwadui FC kuhakikisha unamfukuza koha aliyepo sasa.
Unajua huyu kocha ambaye sasa yupo ndiye alinifanyia fitina hadi nikaondoka pale. Unajua yeye ndiye aliyenifanyia fitna hadi nikaondoshwa kwenye timu.
“Ni mtu ambaye amekuwa akinifuatilia hadi sasa. Kutokana na hali hiyo najua siwezi kukubali kurudi yule akawa yuko pale.
“Mwadui FC wameona kazi yangu, mfano awali nilisikia anasema kuwa sisi tunashinda nyumbani tu, nje hatushindi. Lakini sasa yeye akiwa nyumbani anapigwa, akitoka anapigwa naona wadau wamechoshwa,” alisema Bushiri.

Mwadui FC imekuwa ikienda kwa mwendo wa kusuasua katika Ligi Kuu Bara, jambo ambalo limewafanya uongozi kuchukua hatua mapema.

No comments

Powered by Blogger.