Trump: Muuaji wa Las Vegas ana matatizo ya kiakili

Donald Trump baada ya kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani
Baadhi ya waliohudhuria tamasha hilo wakitoroka kufuatia shambulio la bwana Paddock 

Rais Donald Trump wa Marekani amemtaja muuaji wa watu 59 huku 527 wakijeruhiwa mjini Las Vegas kuwa mgonjwa aliye na akili punguani.

Akizungumza katika ikulu ya Whitehouse , amesema kuwa ataziangazia upya sheria za umiliki wa bunduki katika siku za usoni lakini hakuelezea zaidi.

Maafisa wa polisi wanajaribu kubaini kwa nini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa katika tamasha akiwa katika ghorofa ya 32 karibu na hoteli ya Mandalay Bay.

Polisi walipata bunduki 23 katika chumba chake pamoja na vilipuzi.

Kufikia sasa hakuna sababu mwafaka iliotolewa na wachunguzi hawajapata ishara zozote za shambulio hilo kuhusishwa na ugaidi wa kimataifa.


Baadhi ya wachunguzi wamesema kuwa Paddock alikuwa na historia ya matatizo ya kiakili, lakini hilo halijathibitishwa.

Paddock hajakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu na hakuwa akijulikana na maafisa wa polisi. Haki miliki ya picha FAMILIA YA PADDOCK Image caption Mshukiwa wa mauaji ya las Vegas Stephen Paddock

Akizungumza na wanahabari wakati alipokuwa akijiandaa kupanda ndege ya rais, bwana Trump alisema kuwa Paddock ni mgonjwa wa kiakili .

''Ana matatizo chungu nzima, na tunamchunguza kwa kina'' .

Alipoulizwa, bwana Trump alikataa kuliita shambulio hilo ugaidi wa nchini.

Kuhusu swala la udhibiti wa bunduki, rais alisema: Tutakuwa tukizungumzia kuhusu sheria za bunduki siku sijazo.

Rais Trump ambaye mipango yake kuhusu udhibiti wa bunduki umebadilika katika miaka ya hivi karibuni hakutoa maelezo zaidi.

SOURCE BBC..

No comments

Powered by Blogger.