MBEYA CITY WATAKA UHAKIKA WA BAO LA KICHUYA......
Uongozi wa klabu ya Mbeya City imesema kuwa ina mpango wa kupeleka barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga bao walilofungwa kwenye mchezo uliopita.
Mbeya City wanataka kupata vipimo au uhakika wa bao hilo kama kweli lilikuwa sahihi au la kwa kuwa wanaamini mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga.
Katika mchezo huo Mbeya City walichapwa bao 1-0 na Simba, bao lilofungwa na Shiza Kichuya lakini klabu hiyo imesema kuwa bao hilo siyo halali kwa kuwa mfungaji alikuwa ameotea.
Katibu wa Mbeya City, Emanuel Kimbe amesema kuwa, kwa sasa wanatafakari cha kufanya na baada ya hapo watapeleka malalamiko yao TFF.
“Kila mtu ameona, tafsiri ya offside ni kuingilia mchezo, Kichuya alikuwa offside kabla ya mpira haujamfikia na mpira ulimkuta yeye na kuanza kuukokota na kufanikiwa kufunga.
“Mwamuzi aliyechezesha mechi yetu ndiye aliyechezesha fainali ya FA kati ya Simba na Mbao kule Dodoma na maamuzi yake yalikuwa ya utatautata hivyohivyo na alilalamikiwa, inatupa mashaka na kujiuliza kwa nini inakuwa hivi, lakini tutaangalia na kufanya maamuzi ndani ya saa 72 kuamua kitu cha kufanya kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi lakini kulalamika TFF.
“Ligi imekuwa ngumu na yenye ushindani wa hali ya juu lakini tunapata changamoto ya kimaamuzi kwenye ligi hivyo tunajikuta tunashindwa kufanya vizuri katika baadhi ya mechi,” alisema Kimbe.
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment