''Tunaishemu Mbao na wala Hatuigopi'',,Salumu Nyika...........
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga kinatarajia kuondoka leo jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza tayari kuwavaa Mbao FC wikiendi hii.
Yanga wanasema wako kamili kwa ajili ya mechi hiyo lakini wamesisitiza hawatakuwa na dharau wala kuigopa Mbao FC.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum Nyika amesema wanaujua ubora wa Mbao kwa kuwa ni moja ya timu bora nchini.
“Kitu cha kwanza ujue ni timu ya ligi kuu, tunaiheshimu kama Mbao. Lakini si kwamba tunaigopa kwa kuwa tumejianda ana tuko tayari kwa mechi hiyo,” alisema.
Yanga imekuwa ikijifua bila ya Kocha wake, George Lwandamina ambaye alipata msiba wa kufiwa na mwanaye kwao Zambia.
Post a Comment