Viongozi Wawili CHADEMA Wavuliwa Uanachama.....
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama wawili wa chama hicho.
Waliofutwa
uanachana ni pamoja na aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude
Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona.
Akizungumza
jana Mei 21, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole
Sosopi alisema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote
za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.
Alisema viongozi hao wamehojiwa baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambalo ni kosa kubwa kwenye chama hicho.
Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.
Post a Comment