Haijawahi kutokea Raisi na serikali yake kuheshimu viongozi wa dini'KAKOBE'.....

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema 
kufanikiwa kwa mataifa makubwa kunatokana na kumtanguliza Mungu mbele katika kila shughuli wanayoifanya.

Ameyasema hayo leo Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) iliyofanyika katika Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania(TCRA) jijini Dar es salaam, ambapo amesema jambo hilo limeweza kudhihirika hata kwa nchi ya Marekani kwani uthubutu wao wa kuweka maneno ya Mungu In God We Trust (Tunamuamini Mungu) katika pesa yao ya Dola kumeifanya pesa hiyo kuwa na thamani na kutumika dunia nzima.


“Haijawahi kutokea kuwa na Rais na serikali yake ambao wameheshimu viongozi wa dini kama wewe, si kwa viwango hivi kwa sababu katika uongozi wako hakuna dhehebu kubwa wala dogo wote wameheshimiwa sawa, suala hilo ni ufunguo kwa baraka zinazokuja", amesema Askofu Kakobe.


Kakobe ameongeza kuwa, “Umeanza vyema Rais John Magufuli kwa kumtanguliza Mungu katika shughuli unazozifanya, Mungu ameandaa baraka na zitakapokuja hakuna anayeweza kuzizuia".

No comments

Powered by Blogger.