Chelsea yaukaribia ubingwa, huku Arsenal akiangukia pua
Chelsea wamezidi kujiweka karibu na ubingwa wa ligi kuu Uingereza msimu huu baada ya kuifunga Everton kwa jumla ya mabao matatu kwa sifuri.
Alikuwa nu Pedro, Garry Cahill na Willian ndio ambao walizidi kuipeleka Chelsea karibu na ubingwa wa Epl wakiwa ugenini katika uwanja wa Goodison Park.
Wakati Chelsea wakishinda, Tottenham walikuwa na kibarua kigumu kuwakaribisha majirani zao wa Arsenal ambao wanapambana kurejea katika top four msimu huu.
Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino aliendeleza rekodi yake bora katika derby hiyo ya London baada ya kuibuka kidedea kwa mabao mawili ya Delle Ali na Harry Kane.
Matokeo ya Chelsea na Tottenham yanazifanya mbio za ubingwa kuzidi kunoga kwani tofauti ya alama kati yao inabaki ileile nne huku timu zote mbili zikibakiwa na michezo minne.
Katika michezo mingine Manchester United walishindwa kupanda juu na kukaa katika top four baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja na Swansea wakiwa uwanjani kwao Old Trafford.
Majirani wao wa Manchester City nao walishindwa kuibuka na ushindi dhidi ya vibonde Middlesbrough ambapo City nao walipata suluhu ya bao mbili kwa mbili, shukrani zimuendee Gabriel Jesus aliyewasawazishia City dakika za majeruhi.
Post a Comment