Ajira 4,339 kutolewa kwa Polisi
Serikali ya Tanzaia inatarajia kuajiri watumishi wapatao 4,339 katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka huo wa fedha. “Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ujumla wake, inatarajia kuwapandisha vyeo jumla ya watumishi 7,317.
“Kati yao, watumishi 105 ni wa makao makuu ya wizara, askari 5,772 wa Jeshi la Polisi na askari 1,440 wa Idara ya Uhamiaji alisema Mh. Nchemba
Pia Waziri Nchemba aliitaka serikali iimarishe ulinzi katika wilaya za mkuranga, Kibiti na Rufiji ili wananchi wa maeneo hauo waweze kuishi kwa amani.
credit;bongo5
Post a Comment