Aliyekuwa rais wa Korea Kusini afikishwa mahakamani kuanza kesi

Hii ndio mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu kuondolewa madarakani na kuzuiliwa mwezi Machi mwaka huu. Amekanusha kufanya makosa yeyoteBi Park alifika mahakamani akiandamana na rafiki wake wa karibu, Choi Soon-Sil ambae anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa makampuni makubwa.
Alipofika mahakamani Park Guen-Hye aliulizwa ajira yake na kujibu hana hajaajiriwa.
Yeye na rafiki wake huyo hawakuzungumziana na walikaa kando ya mawakili wao. Rais huyo wa zamani alivalia mavazi meusi na siyo sare za wafungwa ambazo amekua akivalia gerezani
Alikua pia na kibandiko cha nambari yake ya mfungwa 503. Nywele zake zilifungwa kwa kipini kilichotolewa na mamlaka za gereza. Kwa sasa kiongozi huyo anakumbwa na njiya panda baada ya kuondolewa kwenye ikulu.

Post a Comment