Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza




Polisi katika mji wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 19 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa kwenye mulipuko uliotokea ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.

Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.

Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake, wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima.

Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.

Eneo kulikotokea mulipuko huo limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.

Ripoti ambazo hazijathitishwa kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao hawakutajawa zinasema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Ukumbi wa Manchester ambao ulikuwa ukifahamika awali kama ukumbi wa wanaume, ndio ukumbua mkubwa zaidi mjini humo wenye uwezo wa kuwachukua watu 18,000

Barabara ya ukumbi huo unuangana na kituoacha treni cha Victoria kati kati mwa mji.

Ukumbi huo hutumiwa kuandaa tamasha za manyota wakuu kama Ariana Grande nyota wa runinga mwenye umri wa miaka 23 ambaye sasa ni nyota wa muziki wa pop.

No comments

Powered by Blogger.