Balotelli kuwaua Messi na Ronaldo.
Mario Balotelli ” The Black Super Mario” ni moja kati ya wachezaji ambao ni lazima umuone na kumsikia hata kama hutaki kutokana na matukio yake nje na ndani ya uwanja.
Siku za karibuni amekuwa busy na mtandao akishambuliana na watu kwa maneno ikiwemo dongo alilompiga kocha wa zamani wa Liverpool Brenden Rodgers.
Lakini sasa Mario ameibuka na mpya, Baloteli ana mpango ambao anaona kabisa kama huo ukitokea au ukafanikiwa anaweza kuwa mwanasoka bora wa dunia.
Mshambuliaji huyo wa Nice amesema mpango wake ili abebe tuzo hiyo itakuwa ni kumuua tu Crtiano Ronaldo na Lioneil Messi na baada ya hapo kila kitu kitakuwa safi kwake.
Akiongea kwa utani Baloteli amesema “itabidi niwaue hao watu wawili, nimefanya mengi katika soka lakini naona bado nahitaji kufanya mambo mengine makubwa.”
Baada ya maisha yake kisoka kuyumba katika klabu za Liverpool na Man City alijiunga na Nice ambako hadi sasa anaonekana kurudi katika kiwango chake kwani hadi sasa amefunga mabao 15 katika michezo 23.
Post a Comment