Conte: Wenger miongoni mwa makocha bora duniani
Arsene Wenger atasalia kuwa mmoja kati ya wakufunzi bora duniani hata iwapo Arsenal itapoteza fainali ya kombe la FA kulingana na mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte.
Wenger mwenye umri wa miaka 67 amekuwa kocha wa Gunners tangu 1996 na mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu.
Wenger alisema kuwa hatma yake itaamuliwa na mkutano wa bodi ya klabu hiyo baada ya fanaili ya kombe la FA dhidi ya Chelsea.
''Najua vizuri sana kwamba Arsene Wenger amefanya kazi nzuri katika kombe la FA na kushinda mataji mengi'', alisema Conte.
Wenger amekuwa akikabiliwa na pingamizi kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo msimu huu wakimtaka kujiuzulu.
Lakini huenda akamaliza msimu huu na ushindi wa saba wa kombe la FA ikilinganishwa na Liverpool.
Conte anaamini Wenger atakuwa mkufunzi wa Arsenal msimu ujao.
''Sidhani hii itakuwa mechi ya mwisho ya Wenger, anafaa kuendelea kuifunza Arsenal '',aliongezea raia huyo wa Itali ambaye anawania kushinda mataji mawili na Chelsea baada ya kuisadia The Blues kushinda taji la ligi kuu Uingereza.
''Amefanya kazi vizuri. Mara nyengine nchini Uingereza watu wengi wanapuuza jukumu la kuisaidia timu kufuzu katika kombe la vilabu bingwa, "unapokaa sana katika klabu.
''Kwa kweli ni meneja mzuri sana. Anafaa kutambuliwa kuwa miongoni mwa wakufunzi bora dunia katika historia.''
Post a Comment