Safisha safisha ya Pep Gurdiola inaendelea.

Tayari Pablo Zabaleta na Jesus Navas wameshaoneshwa mlango wa kutokea Etihad baada ya kocha Pep Gurdiola kutokukubali viwango vya wachezaji hao.
Pep Gurdiola anaonekana kama anataka kuanza upya kwani toka msimu uishe ni wiki moja tu umepita lakini tayari wachezaji wasiopunguwa wanne wameoneshwa mlango wa kutokea Manchester City.
Sasa baada ya Navas na Zabaleta kuonesha pa kuondokea, beki wa kulia wa timu hiyo Bacary Sagna na mlinda mlango wao Willy Caballero nao wameoneshwa mlango wa kutokea.
Sio hao tu kwani Gael Clichy mlinzi wa kulia wa timu hiyo naye ameoneshwa mlango wa kuondokea Man City baada ya klabu hiyo kutoridhishwa na kiwango chake.
Taarifa rasmi kutoka ndani ya klabu hiyo zimethibitisha kwamba Sagna na Caballero hawatakuwepo Etihad msimu ujao na wanaruhusiwa kuanza kutafuta timu ya kuchezea msimu ujao.
Tetesi zinasema pia mshambuliaji wa klabu hiyo Kun Aguero huenda akaondoka katika klabu hiyo kwani hana furaha na maisha ya klabu hiyo, Aguero muda wake uwanjani umekuwa mdogo tangu Gabriel Jesus ajiunge na klabu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.