JONAS MKUDE WA SIMBA APATA AJARI MBAYA YA GARI WAKATI AKITOKA KWENYE FAINALI ZA F A MJINI DODOMA
Masaa kadhaa baada ya kuiongoza timu yake ya Simba SC kurejea katika anga ya kimataifa kwa ushindi wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC, kiungo wa Simba Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali mbaya akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.
Nahodha huyo wa Simba amepata ajali hiyo maeneo ya Mitibora, Dumila mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kuiwahi Taifa Stars. Taarifa za awali zinasema ameumia maeneo ya shingoni, amekimbizwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wenzie ambao .
Tutaendelea kujuzana hali yake na majeruhi wengine kadri taarifa zitakavyokuwa zinatoka.
Post a Comment