MANGU ATOA YAKE BAADA YA KUAPISHWA KWA SIRRO.............


Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.

Mangu ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuongoza jeshi la polisi nchini.

Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine amesema anamfahamu Sirro kama mchapakazi
mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani.

Alipoulizwa wito wake kwa Sirro kuhusiana na hali tete katika wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, Mangu amesema "Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano."

Sirro ameapishwa leo kuwa IGP, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa polisi (RPC) katika mikoa ya
Tanga, Mwanza na Shinyanga. Baadaye alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa kamishna wa kanda hiyo.

No comments

Powered by Blogger.