Rekodi zinawabeba Arsenal kuwafunga Chelsea hii leo.
Sikia hii, hivi unajua kwamba katika mara nane za mwisho Chelsea kukutana na Arsenal katika michuano ya FA klabu ya Chelsea ilifungwa mara saba?
Na je unafahamu kwamba mwaka 2009 wakati Chelsea walipoifunga Arsenal katika michuano hiyo kwa mabao 2 kwa 1 ilikuwa ndio ushindi wao pekee dhidi ya Arsenal ndani ya miaka 70 iliyopita katika michuano hiyo?
Sahau sasa kuhusu yote hayo ila leo huku Antonio Conte na huku ni Arsenal Wenger wataoneshana nani mbabe kati yao katika fainali ya michuano ya FA mchezo unaoenda kupigwa katika dimba la Wembley.
Wakati Chelsea wenyewe wako fiti 100% kuna tatizo haswa katika safubya ulinzi ya Arsenal ambapo Laurent Koscienly ana adhabu, huku Kieran Gibbs na Shkodran Mustafi wakiwa ni majeruhi.
Kama ni rekodi tu baasi Arsenal wanaweza kubebwa na rekodi kwa maana katika mechi zao saba za mwisho katika uwanja wa Wembley hawajawahi kupoteza hata mchezo mmoja.
Chelsea wenyewe hii ni fainali yao ya saba katika michuano hii ya FA katika karne hii na fainali zao nne za mwisho katika michuano hii walishinda zote na wakishinda kwa tofauti ya bao moja kila fainali.
Toka tajiri Roman Abromovich aichukue klabu hii ya Chelsea imepoteza fainali kubwa mbili tu na zote ikiwa ni 2008,moja ilikuwa UEFA champions nyingine ikiwa fainali ya ligi dhidi ya Tottenham.
Lakini pia kocha wa Chelsea Antonio Conte anaingia katika fainali hizi akiwa hana rekodi nzuri kwani fainali yake ya mwisho kubwa kama kocha ilikuwa mwaka 2012 dhidi ya Napoli na Juve wakifa kwa bao 2 kwa 1.
Post a Comment