SIMBA TARAJIENI MCHEZO WA KIMATAIFA'',MBAO FC
BEKI wa timu ya Mbao FC, Yusuf Ndikumana amesema kuwa klabu ya Simba itarajie kukumbana na kitu cha tofauti kwenye mchezo wao wa fainali ya Kombe la FA ambao unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma baadae leo
. Yusuf alisema kuwa wanatarajia Simba baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu bara akili yao wamehamishia kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA ili wapate tiketi ya kwenda kwenye Kombe la Shirikisho
. “Tunajua namna walivyokamia mchezo huu kwa sababu ni kwa muda mrefu hawajapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ila wanapaswa kujua hata sisi tumejiandaa na wala hautakuwa mchezo rahisi kwao.”
Post a Comment