STAR TIMES YAING'ARISHA SERENGETI BOYS




Kampuni ya ving'amuzi ya StarTimes ni kati ya kampuni zilizojitolea kwa kumwaga kitita cha fedha kusaidia kufanikisha kwa kikosi cha Serengeti Boys.


Serengeti Boys ndiyo wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

Iwapo itaingia nusu fainali ya michuano hiyo, maana yake moja kwa moja inakwenda kufanyika michuano ya Kombe la Dunia itakayochezwa nchini India.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Wang Xiaobo ameongoza timu yake kutia  mchango wa Sh milioni 20 kuichangia Serengeti Boys.


Awali, TFF ilisema inahitaji Sh bilioni moja kufanikisha safari hiyo ya Serengeti Boys ambayo sasa iko nchini Cameroon.

No comments

Powered by Blogger.