Harry Kane kuwavimbia Scotland,,,,
LEO STRAIKA wa Tottenham Harry Kane ndie atakuwa Nahodha wa England wakicheza na Scotland huko Hampden Park, Scotland kwenye Mechi ya Kundi F ya Nchi za Ulaya kusaka kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Hii itakuwa Mechi ya kwanza kwa Kane kuichezea England tangu Septemba 4, 2016 kutokana na kuwa Majeruhi.
Kane atachukua Utepe wa Ukepteni toka kwa Wayne Rooney ambae hakuitwa Kikosini.
Hii itakuwa mara ya 18 kwa Kane kuichezea England tangu alipoanza kucheza Machi 27, 2015 alipoitwa na Meneja wa England Roy Hodgson kucheza dhidi ya Lithuania.
Kane, ambae atakuwa Kepteni wa 119 wa England, ameifungia Tottenham Bao 35 Msimu huu na kuiweka Nafasi ya Pili kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
England ndio Vinara wa Kundi F wakiwa Pointi 6 mbele ya Scotland ambao wako Nafasi ya 4.
KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

MSIMAMO:
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumamosi Juni 10
19:00 Slovenia v Malta [Kundi F]
19:00 Scotland v England [Kundi F]
19:00 Azerbaijan v Northern Ireland [Kundi C]
19:00 Kazakstan v Denmark [Kundi E]
21:45 Norway v Czech Republic [Kundi C]
21:45 Poland v Romania [Kundi E]
21:45 Germany v San Marino [Kundi C]
21:45 Lithuania v Slovakia [Kundi F]
21:45 Montenegro v Armenia [Kundi E]
Jumapili Juni 11
19:00 Moldova v Georgia [Kundi D]
19:00 Finland v Ukraine [Kundi I]
19:00 Ireland v Austria [Kundi D]
21:45 Israel v Albania [Kundi G]
21:45 Iceland v Croatia [Kundi I]
21:45 Macedonia v Spain [Kundi G]
21:45 Italy v Liechtenstein [Kundi G]
21:45 Serbia v Wales Kundi D]
21:45 Kosovo v Turkey [Kundi I
Post a Comment