Mkude awapa masharti Yanga,,,,,
Mkude kwa sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote baada ya mkataba wake na Simba kudaiwa kumalizika hivi karibuni, ikiwa ni mwisho wa mkataba wake wa shilingi milioni 60 aliosaini kuitumikia Simba miaka miwili iliyopita.
Akizungumza na kabasele news kiungo huyo amesema atakuwa tayari kusaini mkataba na klabu ya Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 kwenda juu kutokana na kiwango alichonacho kwa sasa. Simba wamempa ofa ya milioni 40-50 ila yeye amekataa kwa kigezo kwamba mkataba unaoisha walimpa milioni 60 kwa sasa lazima dau lipande.
“Kwa upande wangu nipo tayari kutua Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 na kuendelea hadi shilingi milioni 150 na siwezi kusaini chini ya hapo, nipo tayari kutua katika timu yoyote kwa kiasi ambacho tutakubaliana kwa kuwa kiwango changu kipo vizuri.
Nahodha huyo wa Simba amesema lolote linaweza kutokea kuanzia sasa: “Tusubiri kila kitu kitakuwa wazi muda si mrefu na wadau watajua nitasaini wapi kwa ajili ya msimu ujao, wasiwe na hofu.”
Post a Comment